Ujumbe nilioutuma umekwama angani
Kunani?wingu limefunika kazkazini
Kipepeo nilichokipepesa kinjiani
Kuwa na ari nakwambia atakuwezesha Rabuka

Namwomba Rahima aondoe mashaka
Ninasidi nakusakasaka sadaka
Mola hatanitupa langu litafika
Kuwa na ari nakwambia atakuwezesha Rabuka

Miezi na siku nimevumilia
Naamini dua langu utalikubalia
Usiku, mchana furaha kuipalilia
Kuwa na ari nakwambia atakuwezesha Rabuka
Nimeyaamini ya Rahima kweli mapenzi
Kanitunuku ya kweli kipanzi
Kwake nitavumilia japo ni kazi
Kuwa na ari nakwambia atakuwezesha Rabuka