Namwomba maulana kwa uvumba na ubani
Ndiye wa kweli Rabuka wa vitendo nawambeni
Atakupa kibali muheshimuni jamani
Usitegemee bahati tafuta we vitu vyako
Usitafute mzuri au yule mwenye Mali
Chagua tabia nzuri alotulia akili
Aliyeshika dini na kila siku kuswali
Usitegemee bahati tafuta we vitu vyako
Sina shaka najikimu nangamua kwa upana
Apandacho mwanadamu ndicho atakachovuna
Kuwa na ari nakwambia atakuwezesha Rabana
Usitegemee bahati tafuta we vitu vyako