Giza likiingia mawinguni,ulinifunika
Nilipoanza Julia,nyimbo zilikutoka
Mema ulinipatia,sasa nanufaika
Nikupe zawadi gani mama?
Ulinizaa na kunilea
kunipenda mazuri kuyapokea
Ni zamu yangu kukulea
Nikupe zawadi gani mama?
Natua yangu hatima
Nakupenda sana mama
Hakuna mwingine mwema
Nikupe zawadi gani mama?