Domo domo za nini, huku watia mkono kizani
kisha yakutokea puani, nakuwa na damu ya kunguni
mamako kafanya nini, sasa kalala kaburini
lmepasuka dunia Rabuka tufanyeje?
kisha kuwa kibibi, nakujaa na vimbimbi
lla wapeana chambi, kwa nyimbo zako za harenbii
wastahili maombi, ila si ombi
lmepasuka dunia Rabuka tufanyeje?
kisha Mali kutunukiwa, na shakawa kukuandama
baadaye wachonjomelewa, na machozi kuterema
kisha waaza kutunduwa, kwa kukosa maadili mema
lmepasuka dunia Rabuka tufanyeje?
zangu nne nafunga nikikuacha na USIA
usijaribu bahati kwa kutojua matokeo
shakawa itokuandama ukijifuza kuomba
bahati haivutwi kwa kamba