Leo nazama tungoni,Kalamu nashikilia.
Akili ipo makini,Shairi nakutungia.
Shania niko tabani,Kilio changu sikia.
My enjo my kwini,Mwenzio nakutamani.

Penzi ngano simulizi,Kila mtu ana yake.
Limekuwa jinamizi,Nilalapo nisumbuke.
Ninakiri waziwazi,Bila shaka likafike.
My enjo my kwini,Mwenzio nakutamani.

Meniganda mtimani,Mwengine sitamani.
Ninapokuwa chumbani,Hunijia ko ndotoni.
Nakumisi my hani,wewe kwangu namba wani.
My enjo my kwini,Mwenzio nakutamani.

Huko uliko tambua,Nakuenzi si utani.
Sije ukaniumbua,Nikabaki mashakani.
Nakusihi vumilia,Zitaisha thelathini.
My enjo my kwini,Mwenzio nakutamani.

Written by Poet Jonnie.
Mombasa county.